MARUDIO_KISWAHILI-KIDATO CHA KWANZA_01
MARUDIO _KISWAHILI_KIDATO CHA KWANZA-01
1.Eleza maana ya maneno yafuatayo;
(a)lugha-ni sauti za nasibu
zenye kubeba maana zinazotumika na jamii fulani kwa kusudi la mawasiliano.
>nasibu-hakuna mahusiano ya moja kwa
moja ya neno na kitu.
(b)Fasihi-ni sanaa itumiayo lugha kufikisha ujumbe katika
jamii iliyokusudiwa au husika.
(c)Sarufi- ni mfumo wa kanuni za lugha zinazomuwezesha
mzungumzaji kutunga sentensi sahihi na zenye kukubalika na wazawa.
(d)Kamusi-ni kitabu cha marejeo chenye orodha ndefu ya misamiati
ya lugha Fulani na misamiati hiyo imefafanuliwa kwa kueleza maana zote
zinanazokubalika kwa watumiaji wa lugha .
(e)Nomino-ni neno linalotaja vitu ,viumbe,hali au tendo ili
kuviainisha na kuvitofautisha/kuvipambanua miongoni mwa vitu vingine.
#FOR HOMETEACHING SERVICE CALL/SMS 0622813263

Leave a Comment