Mental block


Je, umeshawahi kukutana na hali yakujiona hukumbukumbi kila kitu au huelewi kila utakachosoma au kuhadithiwa. Umeshawahi kukutana na hali yakusahau  kila kitu pale unapokuwa unaelezea Kitu mbele ya mtu au watu. Na vipi kushindwa kuelewa kile unachokisoma haswa kwa wakati ambao unahitaji uelewe.

Mental block ni hali ya kutokuwa na uwezo wakuelewa au kukumbuka kitu ambayo inaweza mpata mtu kwa mda, inaweza ikawa imechangiwa na kukosa usingizi kwa muda mrefu, kuwa na msongo wa mawazo au kuwaza vitu vyengine tofauti na jambo husika.

Kupitia tafiti mojawapo iliyofanyika ya incubation period yakufikiria njia kabla hujatoa jibu sahihi, ilionesha watu wengi wanaweza kutoa majibu sahihi kwa kipindi ambacho hawana umuhimu nayo hayo majibu au njia za kutatua tatizo haziwahusu kwakipindi hiko.

Kiufupi ilionesha unaweza ukawa na majibu sahihi au mawazo sahihi kwa mda ambao huitaji kuwa na hvyo vitu kwa wakati huo.

Sasa hii hali inatokeaje??
Kuna kitu kinaitwa subconsious mind, hii ni kama benki ya taarifa ambayo inahifadhi kila kitu ambacho umeshawahi kukutana nacho ama kwakukiwaza kukisoma au kukiona na kukihisi. Kupitia subconscious mind sasa ubongo wako huwa unafanya machaguo yakipi kiendelee kukaa kwenye ubongo au kipi kisahauliwe, pia kupitia hii unaweza ukajikuta umepata majibu ya maswali ambayo ulikutana nayo kipindi kilichopita labda tu yakikuwa  magumu ukaamua kuachana nayo lakini ubongo ukaendelea kufanyia kazi na kukupa taarifa kwa kuchelewa.

Inawezekanaje kupotezea kitu kwakuwa kilikuwa kigumu lakini baadae ukaja kupata njia tena bila kuangalia kokote wala kuomba ushauri??
Ubongo wa mwanadamu huwa unapokea taarifa na kuzifanyia kazi takribani million bits 11 kwa sekunde hii inahusisha taarifa kutoka mifumo yote ya fahamu yaani pua, macho, ngozi, ulimi na masikio. Chanzo cha taarifa ni information theory.

Sasa hii inamaanisha kwamba ubongo kama ilivyokompyuta inaratibu mambo yake kwamda ingawa mambo mengi yanaratibiwa kwa mda mchache kuliko kompyuta. Hivyo unaweza ukawa na changamoto yako ambayo umetaka ubongo wako ukupatie jibu wakati huo lakini ikashindikana mpaka baadae wakati tayari huna haja tena na jambo lile ndipo njia au wazo linaletwa na ubongo wako tena. Jambo jepesi ni kwamba hata kama utapotezea jambo fulani tayari ubongo wako ulishaanza kulifanyia kazi jambo hilo kwakulichakata kiufupi tunasema backgroup reflesh ni kama vile baadhi ya simu zinavyoweza kureflesh taarifa bila hata yawewe kujua ukiwa unaendelea kutumia kufanya mambo mengine.

Tukirudi kwenye concept yetu ya incubation period sasa, hii haswa ni nini??
Incubation period ni kipindi ambacho kitu chochote kinahitaji kabla hakijafanya mabadiliko ambayo kinatakiwa kufanya. Kwamfano Wadudu wa magonjwa kama bacteria, virusi kama corona na fungusi wanahitaji mda kwanza wakuzoea mazingira kuzaliana kabla hawajasababisha magonjwa wanapokuwa kwenye mwili wa binadamu. Vivyo hivyo kwenye kufikiria ubongo pia kama tulivyosema unapokea taarifa nyingi sana sana kwa sekunde hivyo nao pia unahitaji mda pia kila wakati kabla hujaweka taarifa nyengine mpya ili kuzichuja taarifa za mwanzo na kuzifanyia kazi kabla haujaziweka kama kumbukumbu katika subconscious mind.


Maisha yetu kiujumla kuanzia tunavyovaa, kuongea, kufikiri na mengineyo mengi ambayo mtu fulani  anaonesha ni matokeo makubwa ya subconscious mind ambayo imeaanza kujengwa toka utotoni ikiwa bado inaendelea kujengeka lakini pia inaweza kubadirika kulingana na taarifa zakila siku ambazo ubongo hupokea.

Tukirudi sasa katika mental block, je ninamna gani unaweza kuzuia hii hali kama huwa inakutokea mara kwa mara katika maamuzi yako?
Ili uweze kuwa na akili yenye kutatua matatizo kwa haraka na wepesi ni muhimu kuijua incubation period ya ubongo wako. Je ni mda gani unatakiwa upumzike kabla hujaanza tena kufikiria au kuwaza  njia za changamoto mbalimbali.. baadhi ya wanasayansi wanasema kwa baadhi ya watu itahitaji dakika kumi tu kuwa pembeni ya tatizo kabla hawajarudi tena na kupata jibu la swala lilokuwa linawatatiza.

Pia kujua ni kitu gani cha kufanya wakati wa incubation period ni swala jengine, kwamfano kuna watu huenda kulala na wakiamka wanakuwa wamepata majibu ya changamoto zao, wengine huenda kupiga stori na wenzao, wengine humwagilia maua, wengine hufanya matembezi hivi vyote na vyengine huwa vinatoa mda kwa ubongo kufanyia kazi jambo ambalo mwanzo lilishindikana kupatiwa ufumbuzi. Sasa hapa ndo unaweza kuona umuhimu wa subconsious mind.

Wanasayansi wanasema uwezo mkubwa wa mtu kuwa attention na taarifa bila kuingiza taarifa nyengine wakati huo ni sekunde nane, kwamaana zikizidi tu sekunde nane utaanza kufikiria labda unawashwa au unafikiria jambo jengine alafu utaaanza kuconcentrate tena hivyo ubungo hufanya switch ya taarifa kila baada ya sekunde kadhaa na hii hutofautiana kuna watu wanaweza kuwaattentive kwa mda mrefu lakini wengine kwa mda mfupi..

Nini chakufanya hapa??
Kwanza hakikisha unapolianza jambo lako jaribu kupunguza msululu wa mawazo mengine kadiri utakavyoweza, punguza kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja fanikisha moja fanya jengine hii huupa ubongo mda wakuchambua taarifa moja moja kwamda unaotosha na kutoa majibu sahihi.

Jambo jengine kila wakati unapofanya mambo yako punguza fikra zakushindwa, punguza kufikiria jambo fulani haliwezekani kama kila mara utakuwa unasema hili jambo ni zuri na naliweza pia utakuwa unachochea ufanisi katika usafirishwaji na uchakatwaji wa taarifa unakuwa unaimarika.

Lakini mwisho kabisa ubongo unahitaji kulishwa taarifa mpya ambazo zinaweza zikakusaidia katika kupata majibu ya maswali utakayokutana nayo baadae hii sasa inahusisha kusoma vitabu kusikiliza  wenye taarifa sahihi au kuona taarifa sahihi..

2 comments:

Powered by Blogger.